RIWAYA: KAMA MAMA KAMA MTOTO

RIWAYA: KAMA MAMA KAMA MTOTO



MWANDISHI: FRANK TITUS

SEHEMU YA KWANZA:

Mama kalolina ni mkazi wa wilaya ya songea, kijiji cha maposeni –peramiho,  yeye ni mjane mwenye mtoto mmoja ambaye ni kalolina, mume wake alifariki miaka mingi iliyopita akimuacha mke na mtoto. Wakati akiishi na mumewe waliishi maisha mazuri mno, kila alichohitaji alikipata kutoka kwa mume wake aliyekuwa mwalimu wa sekondari.
Mara baada ya mume wake kufariki hapo ndipo tabu zilipoanza, walifukuzwa nyumba ya shule waliyokuwa wakiishi, ilibidi yeye na mwanae wapange chumba kimoja. Mbaya zaidi hata mirathi aliyotegemea kuipata kwenye kifo cha mumewe aliambulia fedha kiduchu kutokana na dhuruma za ndugu na wafanyakazi baadhi walioshiriki kula pesa za mirathi.
Maneno maneno yakaanza mtaani, wapo waliosikika wakimsema “ooh amekwisha huyo, alitusumbua sana enzi zake na mumewe, hakujua kuwa mbio za sakafuni uishia ukingoni, tutaona sasa kama maisha hayatomshinda”
Pesa hizo kiduchu alizozipata kwenye mirathi alijitaidi kuwekeza kwenye biashara ndogo ya genge, genge ambalo lilipigwa vita na wanawake wenzie wa mtaa hata baadhi walisusa kununua vitu kwenye genge ilo. Aliishi kwa kuvumilia maneno mengi ya watu, alifanya kila lililowezekana yeye na mwanae wale, alipe pango na mtoto asome.
Maisha yalianza kumuelemea, genge lilikosa wateja, pesa ya kodi ilikosekana,  chakula kilianza kusumbua ndani ya nyumba, kuna siku zilipita kwa mlo mmoja, aliishi kwa kukopa kwa majirani lakini mwisho wa siku hata majirani walimchoka, hapo ndipo kichwa cha mawazo kilianza kumsumbua.
Siku moja akiwa anawaza atafanyaje kuepukana na hali yake ya maisha, mara akasikia mdundo mkubwa wa ngoma na sauti ya watu wakiimba “usengwilee wanachama, usengwile akina mamaa” na punde akasikia;
“Akina mama oyeee!” sauti ya kike ilisikika
“oyeee!” watu walimjibu
Mama kalo alishtuka na kusimama, akatupia macho mbele…

inaendelea....#letusshine

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01

TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01