Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2019

SIRI YA MAFANIKIO

JIAMINI, WEWE NI SABABU. Ukiusikiliza wimbo wa HARMONIZE -NEVER GIVE UP kuna sehemu utasikia akisimulia namna alivyoenda kushindana katika mashindano ya kuimba ya BONGO STAR SEARCH (BSS)  na akaambiwa hajui kuimba. inaonekana harmonize mwenyewe alijiamini kwamba anajua Sana kuimba,  lakini waliomsikiliza walaikataa wakidai hajui. LAKINI,  Leo hii HARMONIZE akitoa nyimbo hata wale waliokuwa wakimdharau kuwa hajui,  wanacheza nyimbo zake na wanatamani kuwa Kama harmonize . NDIVYO ILIVYO;  katika haya maisha ni ngumu Sana mtu kuamini kipaji au uwezo wako. Hata Kama wewe mwenyewe unajiamini na unajikubali lakini ukiwaonyesha watu kwamba unauwezo flani, hawatokuamini, watakuambia unapoteza mda,  hufai. HATA kwa wajasiriamali,  mwanzo uwa mgumu Sana,  utakuta kuanzia wajasiriamali wenzio, wateja hata wapita njia WOTE HAWAKUAMINI,  tena wengine wataona hufai kuwa mjasiriamali. KUMBUKA;  ukiruhusu tu kuwapa nafasi katika akili yako UMEKWISHA,  UMEPOTEA,  HUO NDIO UTAKUWA MWISHO WAK

UNAJUA NINII?

BLOG YANGU MPYA: karibuni nyoteee katika blog hii mpya ya LET US SHINE ikiwa na maana acha tung'ae/acha tupendeze n. k. Kwanini let us shine.... NATAKA TUBADILISHANE MAWAZO YA MAFANIKIO.... UMU KUTAKUWA NA..... 1.makala mbalimbali 2.stori Kali,  tamthilia,  riwaya,  chombezo,  hadithi n.k 3.music audio and video 4.na mengine mengi tuuuu ikiwemo ANY BREAKING NEWZ..... ASANTENI NA KARIBUNI KUCHANGIA

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01

Picha
CHOMBEZO:BAD FEELINGS (hisia mbaya) MWANDISHI: FRANK TITUS-MANSHYNE AGE: 18+ sehemu ya 01: Tamaa utumwa na hisia,  hisia nazo uongozwa na vijimawazo flani hivi ambavyo vikiamua kukuendesha basi utaenda tu. Watu wengi wanasema akili ya mtu ipo katika ubongo wake,  labda ni kweli na ndio maana hata mawazo utoka uko uko,  hata matendo yote tuyafanyayo ni kutokana na hisia zetu,  lakini utata upo pale tu hisia zikiwa mbaya.... Ni rahisi Sana hisia zako kutamani kuwa na tabia njema,  lakini ni rahisi Sana hisia zako kukufanya uonekane huna tabia njema. Na siku zote majaribu umkuta Yule hasiyeyataka.  Kosa moja goli moja, unatumia kiungo chako mwenyewe kutamani kiungo cha mwenzio,  unatamani kutulia lakini hisia sasa, hisia zako hazitaki. ILIKUWA Ni katika shule ya mchanganyiko wasichana na wavulana kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita, (KIORORO HIGH SCHOOL). Licha ya shule hiyo kufahamika Sana kitendo kilichopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao,  na wanafunzi wenyewe kuic

TAMTHILIA: MOON OF MY LIFE (MML) sehemu ya kwanza

TAMTHILIA: MOON OF MY LIFE (MML) Mtunzi/mwandishi: manshye *************************************** Episode 01 Ni baada ya kumaliza chuo, kijana aliekuwa mtu pendwa chuoni kutokana na utanashati wake, akili yake ya darasani na kujitambua kimaisha, upendo na ushirikiano wake kwa vijana wenzie wa jinsia zote, upole, ukarimu na uchangamfu wake kutokana na mazingira zilikuwa sababu tosha za mtu huyo kupendwa. Licha ya sababu nyingi, walizoea kumuita handsome boy kutokana na sura yake na staili ya nywele zake kufanana na mcheza mpira wa miguu maarufu kwa jina la neymar jr pamoja na muigizaji maarufu wa bongo movie aitwaye rammy galis, hata yeye mwenyewe aliwapenda sana hao watu. Lakini pia alishawai kuitwa fonsi, hii ni kutokana pia na stahili na mbwembwe zake kufanana na muimba muziki wa nchini pueto rico, luis fonsi, aliyetamba na wimbo wa despacito, Kijana huyo sio mwingine bali ni kaxoghur santos jr. Sifa zake hazikuishia chuoni, hata mara baada ya kurudi kwao dar es salaam, vijana

TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01

TAMTHILIA: CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (CPL) (MTU ALIETHIBITISHWA KWA MAISHA YANGU) MWANDISHI: MANSHINE Email address: manshinef@gmail.com instagram: @manshynee           facebook @let us shine Episode 01 . VENUE: Ilikua ni muda wa kipindi cha ujasiriamali kwa wanafunzi wanaosomea biashara., lecturer (mwalimu wa chuo) akiwa mbele ya venue akifundisha. Kutokana na ukali wa lecturer yule darasa lilikua kimya sana hali iliyopelekea wanachuo kuwa waoga kwasababu walishaambiwa katika kipindi chake kuleta fujo au kelele ni sawa na kujiondoa chuoni hapo. Frank akiwa ni mmoja wa wanachuo alikua makini sana kusikiliza. Ilifikia hatua akawa anatikisa kichwa kuonyesha jinsi gani alikua akielewa katika kipindi hicho. Wakati kipindi kikikaribia kuisha, mkufunzi (lecturer) aliuliza swali… “wanafunzi Nani anapenda kuwa mfanyabiashara., na kwanini? Na mtaji utaupata wapi? loveness akanyosha mkono, akaambiwa ajibu swali… LOVENESS: mimi sipendi kuwa mfanyabiashara kwasababu bia