Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2020

TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.

Picha
UCHUMBA Unaanzaa siku Mungu amekuthibitishia kuwa huyo ndiye na huyo mtu akakubari uwe mchumba wake. au uchumba unaanza siku ambapo hao wawili wanakubaliana wawe wachumba. Basi Hapo mnakuwa wachumba lakini mbele za Mungu tu na sio kwa wanadamu Mungu anaheshimu maagano ya wanadamu. Hivyo kama umeingia kwenye mahusiano na mtu ambaye sio sahihi, Mungu hataingilia hayo maagano yenu. Au kama wewe sio mkaidi basi kwa rehema zake atayavunja hayo mahusiano. Asema “Aondoa [agano] la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.”(Ebr 10:9) Lakini Mungu ametaka uchumba utambulike na mbele za wanadamu pia. Hivyo kinachofuatwa ni kuuweka huo uchumba unaotambulika na Mungu waziwazi mbele za wanadamu kwa njia sahihi. Kanisani, kwa wazazi, n.k.. Kwa wazazi kuna njia nyingi za kuwa wachumba Ambayo kwa familia nyingi kwanza ni kutoa Posa(au kujitambulisha kwa wazazi rasmi), kisha kutoa mahali(kwa ambao ipo). Lakini kwa wale wenye mambo ya Kutoa Posa; mbele za Mungu uchumba unaishi