TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.


UCHUMBA Unaanzaa siku Mungu amekuthibitishia kuwa huyo ndiye na huyo mtu akakubari uwe mchumba wake.
au uchumba unaanza siku ambapo hao wawili wanakubaliana wawe wachumba.
Basi Hapo mnakuwa wachumba lakini mbele za Mungu tu na sio kwa wanadamu
Mungu anaheshimu maagano ya wanadamu.
Hivyo kama umeingia kwenye mahusiano na mtu ambaye sio sahihi, Mungu hataingilia hayo maagano yenu. Au kama wewe sio mkaidi basi kwa rehema zake atayavunja hayo mahusiano.
Asema “Aondoa [agano] la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.”(Ebr 10:9)
Lakini Mungu ametaka uchumba utambulike na mbele za wanadamu pia.
Hivyo kinachofuatwa ni kuuweka huo uchumba unaotambulika na Mungu waziwazi mbele za wanadamu kwa njia sahihi.
Kanisani, kwa wazazi, n.k..
Kwa wazazi kuna njia nyingi za kuwa wachumba
Ambayo kwa familia nyingi kwanza ni kutoa Posa(au kujitambulisha kwa wazazi rasmi), kisha kutoa mahali(kwa ambao ipo).
Lakini kwa wale wenye mambo ya Kutoa Posa; mbele za Mungu uchumba unaishia mtu ukishatoa Posa.
Ukishatoa Posa(Arabuni ya ndoa) mbele za Mungu anakuwa mke wako.
Lakini hii mbele za wanadamu bado sio mke wako.
Na hata mbele za Mungu bado ndoa haijakamilika Ingawa huyo bibi harusi Mungu atamwita mkeo.
Na katika hicho kipindi ikitokea ukifanya naye mapenzi huyo mtu utakuwa mzinzi mbele za Mungu.
Mungu hakuruhusu umguse kwanza.
maana bado ukifanya hivyo utakuwa umeanguka katika dhambi ya uzinzi.
Angalia haya meneno yafuatayo…
Mathayo 1:18-20 Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Hapo tunaona.. Ingawa Mungu anamwita mkewe, lakini bado hajawa mkewe rasmi kwa jinsi ya ndoa.
Ndio maana hakuweza kumkaribia mariamu mpaka siku ndoa ifungwe rasmi.
Kumbuka hata Kanisa ni Bibi harusi wa Yesu. Lakini linaitwa mke wa Yesu.
Ufunuo 21:9 Akaja mmoja wa wale malaika saba,…, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.
Umeona hapo?. Bibi harusi tayari kwa kufunga ndoa Rasmi pia anaitwa mke.
Lakini hapo bibi harusi anao uwezo wa kuvunja mahusiano kabla ya Ndoa.
Hata sisi sasa ni mabibi harusi wa Yesu Kristo. Lakini mtu anaweza kumwacha Yesu wakati wowote.
Mpaka tutakapopewa miili mipya isiyoweza kutenda dhambi. Ndiyo ndoa ya milele na milele asiyovunjika.
Paulo Anasema “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Sasa umeposwa. Simama katika huo uaminifu hata Yesu atakapotupa miili mipya isiyoweza kutenda dhambi.
___________________
Mhuri wa Pili wa uchumba ni pale unapokuwa umetoa Mahali (au unapokuwa umekabidhiwa rasmi na wazazi au ndugu zake)
Sasa hapo kwa wanadamu kwa kanuni hiyohiyo ya Mungu uchumba ni pale unapotambulishwa rasmi kwa wanadamu kuwa ninyi wawili ni wachumba.
_________________________
Hapo ndipo mnakuwa wachumba mbele za Mungu na Mbele za wanadamu.(ingawa kwa Mungu tayari ni mke na Mume ambao bado wanaweza kuachana).
Mungu anataka tufanya haya mambo kwa kumpendeza yeye na wanadamu pia.
“Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu”(Luka 1:52)
Hapo ingawa Mbele za Mungu ni mke na Mume (kabla ya kufunga ndoa rasmi) lakini mbele za wanadamu ni wachumba…
na mkikutana kimwili hiyo bado unakuwa mzinzi mbele za Mungu na mbele za wanadamu
Kumbuka Hapo Bado wapenzi hao wanao uwezo wa kuyavunja hayo mahusiono pasipo dhambi.
Hivyo ni dhambi kuunganisha miili yenu kabla ya ndoa rasmi. Ni uzinzi.
Ndio maana Bado hamhuruhisiwi kujiunga miili yenu kwa tendo la ndoa.
Maana tendo la ndoa ni kwa ajili ya wale ambao wamekuwa mke na Mume kwa sheria ya kutokuvunja ndoa.
Maana Mkifanya hivyo kabla ya ndoa mtakuwa mmezini bado.
See 1kor 7:36-38
_______
Baada ya hapo Ndoa inafungwa kwa Neno la Bwana.
Na kutiwa mhuri kwa Tendo la Ndoa kuwa mwili mmoja.
Kwa sheria isiyo ya kubadirika.
Hadi hapo ndoa hiyo hakuna aweza kuivunja zaidi ya kifo.
Hapo ndipo mtakuwa mme na Mke mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Pasipo dhambi.
1kor 6:16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
Nanyi mnafanywa mwili mmoja kwa njia ya Tendo la Ndoa.
Hapa huwezi kuvunja ndoa hiyo mpaka kifo.
Marko 10:9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
ANGALIZO.
Wakati wa Uchumba;
Kama unazini na uko kwenye dhambi ya uzinzi na huyo mchumba wako kabla ya ndoa na ukaenda kufunda ndoa huku tayari mnazini kama kawaida; zile baraka za ndoa hugeuka kuwa laana.
Mungu hadhihakiwi.
Unaweza kuwadanganya wachungaji, lakini sio Mungu.
Yakobo alisema “Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka(Mwanzo 27:13)
Hivyo watumishi watakubariki siku hiyo lakini zile baraka hugeuka kuwa laana.
Maana Ndoa ni utakatifu wa Mungu (Malaki 2:11)
Na yeyote anayeshiriki na kuingia kwenye ndoa isivyosahihi hugeuka kuwa laana.
Hivyo angalia saaana wakati wa uchumba usije ukaharibu mema ya ndoa yako na kuifunga ndoa katika laana badara ya baraka. 1Kor 11:26-32

Frank Titus Kapinga. 
#shared

Maoni

  1. Asante @frank kwa somo uliloliandaa maana hii dhambi ya uzinzi ni kubwa na inazidi kututafuna kwa kweli, kumbe tunajipunguzia baraka kwa mikono yetu na akili zetu timamu alafu baadae tunasema tumerogwa kumbe ni laana tunatembea nazo.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01