TAMTHILIA: CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (CPL) SEHEMU YA 2-5

TAMTHILIA: CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (CPL)

MWANDISHI: FRANK TITUS -MANSHYNE

Episode 02.

MARIA: hospitali wanasema ni maumivu ya kichwa yalimzidi. Na inasemekana chanzo ni wewe?
FRANK: kwahyo hata wewe maria unaamini mimi ni chanzo?
MARIA: sasa chanzo ni nani? lakini ni Kutokana na yale uliyoongea class.
FRANK: kwan niliongea vibaya?
MARIA: hapana ulikua sawa lakini ndo hivo mtu yupo hospitali….
FRANK: ok fresh, wacha mimi nikale alafu nishachoka nataka nikapumzike hostel. Aliongea frank huku akisimama na kuondoka.
MARIA: wewe ina maana huend hospital kumuona? Wewe frank? Mmh makubwa!
*************************************************************
Loveness akiwa hospital alitembelewa na marafiki zake pamoja na wanachuo wengine. Baadhi walimletea zawadi kama juice, biscuit na matunda. Aliwashuukuru sana.
“Lakin vipi saiz unaendeleaje?” aliuliza issa
LOVENESS: kwa sasa naendelea vzr, docta kasema leo naweza kuruhusiwa
ISSA: kwan tatizo lilikua nini?
LOVENESS: ni kichwa tu ila sasa Niko poa
ISSA: kwahyo kesho utakuja pindi?
LOVENESS: nitaangalia!
Basi mara akaingia docta, akawaomba wanafunzi wampishe ili aongee na mgonjwa wake
DOCTA: kama nilivosema, jitahidi kupunguza mawazo. Mara nyingi mawazo ndo sababu kubwa ya maumivu ya kichwa. Pia hakikisha unakunywa maji mengi na kufanya mazoezi ili mwili upate afya bora na nguvu. Usisahau kuwa kukaa sana peke ako ni chanzo cha kuanza kufikiria hata mambo yasiyo ya msingi. Na mambo hayo ndio uleta stress. Docta akamaliza na kumruhusu kutoka pale hospitali.
Loveness na Rafiki zake wakapitia mapokezi na kuaga kwa sababu alikua akitumia bima ya chuo basi matibabu yake yalifanyaka bila malipo.
***********
Frank yeye bila wasiwasi alikua hostel kwake akijisomea. Mara akaingia Rafiki ake rama.
RAMA: kwa raha zote, kaka hivi hata hujishtukii?
FRANK: kujishtukia kwa lipi?
RAMA: we si umempa ugonjwa wa kichwa mwenzio, au ulimpa makusudi? Akaongea rama huku akicheka
FRANK: ah kausha sio kila mtu lazma aende, wengine tutamuombea tu kwa mungu atapona.
RAMA: dah tena unajibu utafikiri wewe sio chanzo haya bhna.
FRANK: we kama ulienda poa. Mi Siwez kwenda.
Basi siku hyo nayo ikapita, frank hakwenda kumuona loveness. Watu wengi hawakupenda kile kitendo na kila aliemuuliza kwan hakwenda alijibu kirahisi tu “kuna vitu vingi vya kufanya atapona tu”.
Loveness yeye baada ya kuruhusiwa akarud hostel na kulala. Rafiki zake walikuja kumtaka hali wakimletea na zawadi. Ikawa kila alemuuliza kama kesho yake ataingia pindi, alijibu tu “nitaangalia”.
***********
Ikawa ni siku nyingine tena asubuhi katika kipindi cha uchumi. Darasa lilionekana kujaa huku wanachuo wakijadili mambo mbalimbali. Lakini hata hivyo macho ya watu wengi yakawa yanawatafuta frank na loveness ambao hawakuonekana mule darasani.
ISSA; naona pasua kichwa hafiki leo, au nae anaumwa?
MARIA: achaga unafki na wewe. Mwalimu tu bado hajafika mda bado
ISSA: mda bado kivipi? Wakati yeye kila siku uwa anakua wa kwanza kuingia pindi, tena anakaa viti vya mbele.
Wakiwa bado wanamjadili mara frank huyo akawa anaingia class, mara nyingi anakaaga mbele ila Kwakuwa alichelewa akakuta mbele kumejaa na nyuma kumejaa. Baada ya kuangalia vzr akaziona siti mbili zikiwa hazina watu, akaenda na kukaa siti moja. Ile anakaa tu na mwalimu wa uchumi akaingia, ukimya ukatawala.
MWALIMU: natumaini kila mtu ameingia, hivyo CR (kiongozi wa darasa) naomba ukafunge milango yote.
CR akatoka na kwenda kufunga mlango, akafunga wa mbele na akaelekea nyuma ili akafunge mlango wa nyuma. Bila matarajio ya watu wengi ile anataka kufunga mlango tu na loveness akaingia watu wote wakageuka kumuangalia.
Loveness akaanza kutafuta nafasi ya kukaa, akaiona akaanza kuisogelea ili akakae. Alipoifikia akaganda kama sekunde kumi hivi akitafakari, akajiiuliza atakaaje na mtu asiyetaka hata kumuona? kwa makusudi akapitiliza hadi mbele na kukaa kwa kubanana na Rafiki zake.
Kitendo kile kilizua minong’ono ya chini chini mule ndani hadi mwalimu alipoongea
MWL: darasa naomba utulivu. Nafikiri hakuna asiyejua kushuka kwa uchumi wa nchi. Uchumi wa nchi unategemea sana biashara mbalimbali za wananchi wa nchi husika. Mfano kupitia kodi na tozo mbalimbali. Kama wananchi wasipofanya biashara na kuichangia nchi yao kupitia kodi hizo basi lazima uchumi ushuke. Lakini pia biashara hizi za wananchi zinachangamoto nyingi, changamoto hizo ndizo zinazowafanya watu kukwepa kodi. Sasa kila mtu aandae karatasi moja, na aniandikie ni changamoto zipi zinazowakabili wafanyabiashara hadi washindwe kulipa kodi? Natoa dakika 10 tu kwa zoezi hili.  Akikisha unaandika jina lako na namba ya usajili.
Basi kila mtu akaandaa karatasi na kuanza kuandika alichofikiria kuhusu swali lile. Watu walikua busy na kujibu swali hadi dakika kumi zilipofikia.
MWL: natoa dakika 2 za kukusanya, kunja karatasi yako alafu mpe wa mbele yako nae ampe wa mbele yake hadi zifike kwangu.
Karatasi zikakusanywa na kuwekwa kwenye kibox, alafu mwalimu akatangaza tena
MWL: sasa nitapita na hichi kibox, kila mtu ataingiza mkono na kuchukua karatasi moja alafu badae atapita mbele kutusomea majibu ya mwenzie.
Zoezi likafanyka haraka, na badae mwalimu akatangaza
MWL: kila mtu afungue karatasi yake ili amjue mwenzie kabla hamjaanza kupita mbele.
Frank akafungua haraka karatasi yake akaangalia jina la mwenzie akakutana na maneno “LOVENESS JOHN” akavuta picha kama darasa lina loveness mwingine lakini akajisemea moyoni “atakua yule yule, sasa si balaa lingine hili. Au nibadili karatasi? Lakin ticha alisema akimuona mtu anabadili karatasi atapata tabu, duuh sijui bhana itafahamika tu”
Watu wakawa wanacheki maratasi yao, maria akaangalia akakutana na jina asilolijua akakausha., issa akaicheki nae akakuta jina asilolijua akakausha.
Loveness kabla hajafungua lake akaanza kuchungulia karatasi za wenzie kwanza, badae akaanza kulifungua karatasi lake kwa manjonjo na madoido yotee uku akiwaziba wenzie wasione, macho yalimtoka na akaganda baada ya kukutana na jina “FRANK KAKOLANYA”

Episode 03.

macho yalimtoka na akaganda baada ya kukutana na jina “FRANK KAKOLANYA"
Frank akafikiria sana kubadilisha karatasi yake kwa mtu wa pembeni yake, lakin akaona sio tabu maana ile ndio sehemu ya shule akaacha. Loveness yeye alitamani hata kuichana ile karatasi alichukia sana, alijiona kama alikosea katika kuchagua karatasi. Akamshtua Rafiki ake wa pembeni
LOVENESS: sarah, sarah pliiiz nakuomba tubadilishane karatasi (aliongea loveness kwa sauti ya chini)
SARAH: hapana love mwalimu atatuona. Kwan hiyo ina nini?
LOVENESS: sarah nakuomba mwaya nisaidie. Mwalimu hawez kutuona
SARAH: mmh ilete bas fanya fasta…. (aliongea sarah huku akanyosha mkono kuipokea).
Basi kwa siri wakabadilishana zile karatasi., loveness moyo wake ukatulia. alitokea kumchukia sana frank. Alijiambia moyoni “yani nianze tu nipite mbele, eti nisome karatasi ya yule shetani, watu wakiwa wakinisikiliza looh labda mimi sio love”.
Wakati wanafunzi wakimsubiri mwalimu nini aseme, mara mwalimu akatoka kule mbele na kuanza kuzunguka kwa kila mtu mule ndani, akazunguka darasa lotee huku akiwa siriazi, usoni alionyesha kuchukua sana. Hakuna aliejua amechukia kwa ajili gani. Lakini ghafla mwalimu alikuja kusimama kwenye kiti cha loveness na Rafiki zake, akaongea
MWL: wewe dada mwenye nguo nyeupe ebu simama. (alimsimamisha sarah). Sarah alianza kuogopa, akajua kimeshanuka, akawa anatetemeka.,
MWL: humu ndani nyie wote ni watu wazima, hadi mmefika level hii inaonyesha ni jinsi gani mna uelewa mkubwa. Sasa nashangaa sana kwanini kuna Bahadhi ya watu bado hawaelewi. Na wewe dada hapo ulievaa nguo nyekundu nawe simama!. (huyo sasa alikua loveness)
MWL: nipeni jibu sahihi kwanini mmebadilishana karatasi? au mlijua mnafanya siri? Mimi nilianza kuwaona mda mrefu niliwaacha kwanza. (walikua kimya, walionyesha wazi kwamba ni kweli walibadilishana).
MWL: sasa ebu rudishianeni karatasi haraka. (loveness akiwa anaogopa, akarudisha lile karatasi na kuchukua lake). Alafu wewe mwenye nyeupe nenda kakae pale (aliambiwa sarah akakae kwenye ile siti karibu na frank). Alafu wewe mwenye nyekundu ndo utakuwa wa kwanza kupita mbele ukatusomee majibu yako (loveness akaona kumekuchaaa).
Loveness akapita hadi mbele ya darasa ambako alipanda juu kwenye stage ambayo kila mtu alikua anamuona. Alitulia kimya akiwa na hasira, macho yote akitazama chini. Alimchukia sana mwalimu, akataman hata atoke mule darasani lakin ndo hivo tenaaa.
MWL: kabla hujatusomea mwenzio wa kwenye karatasi, kwanza jitambulishe mwenyewe unaitwa nani.
LOVENESS: loveness john (alijitambulisha love kwa upole kabisa).
MWL: haya tusomee jina la mwenzio kwenye karatasi ili nae apite mbele…...
LOVENESS: (akiwa kama hataki, ila kwa amri akataka) anaitwa FRANK KAKOLANYA.  (baada ya kutaja tu hilo jina na minong’ono ikaanza mule ndani, kuna watu walicheka, wengine wakatabasam maana walijua kitakacho tokea).
ISSA: aah ndio maana love alibadili karatasi, duuh hata ningekua mimi mbona ningelichana kabisaa.
MARIA: we nae kama mwanamke mambo yako. Basi kuwa wewe si unataka uwe mwanamke.
ISSA: kausha basi na weweee.
MWL: naomba utulivu. alafu frank kakolanya ningependa usimame ulipo na upite mbele…... (frank akasimama na kwenda kule mbele ambapo alikaa mbali kidogo na loveness).
MWL: frank nawewe fungua karatasi, alafu tutajie jina la mwenzio. Nataka tufanye mambo kwa haraka….
FRANK: anaitwa LOVENESS JOHN. (mwalimu akashangaa, loveness pia akashangaa, hata darasa zima likashangaa. Hawakuamini walijua labda frank anatania. Watu wakajiuliza “inawezekanaje hii”? …).
MWL:  frank ebu nipe karatasi yako, haiwezekani. (mwalimu baada ya kuchukua karatasi ya frank akakuta ni kweli LOVENESS JOHN). Akacheka akiwa kama haamini vile. Akastaajbu sana.
MWL: basi sawa nafikiri hii itakuwa nzuri kwa sababu tutasikia majibu kutoka kwa hawa wote, au sio wanafunzi…? (aliongea mwalimu pasipokujua wale kwasasa ni zaidi ya wapinzani wa jadi).
WANAFUNZI: “Ndioooooooooooo” (watu si walijua mambo leoo, pia kama ujuavyo hakuna mwanafunzi anayependa kupita mbele ya darasa kwahiyo watu waliitikia kwa moyo wote).
MWL: sasa nilitaka aanze loveness, lakin utaanza wewe frank kutusomea majibu ya loveness.
FRANK: (akamcheck kwanza loveness akamuona ameangalia pembeni tena akionyesha wazi hajapenda kinachoendelea, akafungua karatasi na kuanza kusoma majibu ya mwenzie). Ameandika hivi “changamoto kubwa kwa wananchi katika biashara ni ELIMU YA KUTOJITAMBUA. Watu wengi wanakurupuka katika kufanya biashara, wao wanadhani biashara ipo kwa ajili ya kila mtu. Matokeo yake hawapati chochote katika hizo biashara hali inayopelekea wao kukwepa kodi, pia sababu ya pili ni umri, watu hawazingatii kabisa swala la umri. Wao wanadhani watoto, vijana hata wazee wote wanaruhusiwa katika biashara. Matokeo yake watoto wengi hawana elimu ya kulipa kodi, vijana wengi wanatumia madawa na pombe hivyo wanakwepa kodi, na wazee wengi wao wanashindwa kufanya kazi kwa ufasaha hivyo wanashindwa kulipa kodi. “frank akamaliza kusoma yaliyomo…….
Wanafunzi wote kimyaaaa, wakitafakari maneno hayoo, mwalimu mwenyewe akawa hana neno kwa muda huo akawa anatabasam tu…. loveness yeye alikuwa kimya, sio kwamba alikua hasikilizi, alisikia kila kitu alichokiandika, alisubiri tu mwalimu aongee…...
MWL: NADHANI wote mmesikia vzr majibu ya loveness. Sasa kabla sijaruhusu maswali, naomba loveness na wewe tusomee majibu ya frank. (aliongea mwalimu huku akimcheck loveness ambaye bado alikua anaangaalia kwa pembeni).
LOVENESS: (akafungua karatasi na kuanza kusoma majibu ya frank). “ wafanyabiashara ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi, bila wao nchi haiwezi kuendelea. Katika biashara watu wanakutana na changamoto kubwa ikiwemo 1. Kushuka kwa thamani ya fedha, kama fedha ikiwa haina thaman katika nchi ina maana itakuwa ngumu sana kwa mfanyabiashara kupata faida kwa sababu pesa kwake itakua ngumu kupatikana. 2. Ukubwa wa kodi, kodi inatakiwa isiwe inayodhidi mapato ya watu, hakuna mtu atayekubali kulipa kodi kubwa inayodhidi kile anachokipata. 3. Elimu kuhusu kodi, inawezekana watu hawaelewi chochote kuhusu kodi. hakuna mtu anayelipia kitu bila kujua umuhimu wa kitu hicho, wafanyabiashara ambao ndio walipa kodi wanatakiwa wapewe elimu kuhusu umuhimu wa kodi wanazozilipa. 4.sera ya ulipaji kodi, hili ni tatizo kubwa kwa wananchi, Mfano kama sera itataka kila biashara illipe kodi basi watu watakwepa kodi. Kwa sababu kuna Bahadhi ya biashara ni ndogo sana tena zenye kipato cha chini, kumlipisha kodi mfanyabiashara wa namna hyo ni sawa na kumkandamiza. Sera inabidi iandae mfumo mzuri utakaoonyesha ni biashara za namna gani zilipe kodi ili kila mtu ajue akifikia hatua Fulani ya biashara itabidi alipe kodi”. Loveness akamaliza kusoma majibu ya frank…
Mara tu baada ya loveness kumaliza kusoma, darasa zima walisimama na kuanza kupiga makofi kuonyesha ni jinsi gan frank alijibu swali lile kwa umakini na usahihi sanaaa, bila kutegemea mwalimu nae akaanza kupiga makofi huku akimsifu sana frank…frank akafurahi sanaaa.
Lakini upande wa pili kwa  loveness hali ilikua ndivyo sivyo…………...

Episode 04.

 loveness alichukia sana, alichukia kwanini yeye hakupigiwa makofi na frank apigiwe, kwa hasira akaweka lile karatasi la frank kwenye meza na kuanza kushuka chini kuelekea kwenye kiti chake, ile anataka kukaa tu…
MWL: loveness bado hatujamaliza, ebu rudi hapa haraka….
Loveness kwa hasira akasimama tena na kurudi, hakutaka hata kumuangalia mtu akawa anaangalia pembeni kabisa, kwenye ukuta.
MWL: wanafunzi naruhusu maswali manne tu. Mawili kwa loveness na mawili kwa frank.
Baada ya mwalimu kuruhusu maswali, issa alionekana kufurahi sanaa
MARIA: we naye vipi mbona unafurahi hivo baada ya mwalimu kuruhusu maswali?
ISSA: acha tu nina hasira na huyo frank, haiwezekani kila siku anamuumiza loveness
MARIA: kwahyo unatakaje?
ISSA: subiri, swali nitakalomtandika labda aje kusaidiwa na malaika. (aliongea issa kwa sifa).
Ni kweli issa akanyosha mkono, mwalimu akamruhusu aulize swali lake……
ISSA: swali langu ni fupi tu na nataka nijibiwe na frank, “kama kila mtu atayependa biashara atafanikiwa naomba unitajie biashara tano ambazo mtu akifanya hawezi kupata hasara”
“Mmh” watu waliguna maana swali limekaa kwa kukomoa alafu aliendani na somo la siku hyo.
Frank alilisikia swali vizuri tu, lakini akashangaa swali lipo nje ya mada, hakujua kama anakomolewa maana yeye si mtu wa kuwaza vitu tofauti. Hakusita kujibu, alijibu swali kama ifuatavyo……
FRANK: siku zote ukipenda unachofanya basi kitakupa unachotaka hivyo basi hata biashara ukiipenda lazima ikupe mafanikio. Kuna biashara nyingi mtu anaweza kuzifanya na zikampa faida lakini kumbuka hata mwizi anapenda kuiba lakini sio kila anapatoka kuiba uwa anafanikiwa, msaanii anapenda sana kazi yake lakini sio kila akitoa nyimbo itafanya vizuri. Hivyo hivyo katika biashara, siku zote biashara haina hasara ila hasara ni matokeo ya biashara. Na katika biashara ukiona unachokifaya hakikupi hasara ujue unalolifanya sio sahihi kwako. Lazima uipende hasara ili ikukumbushe faida. Je wewe unataka kusema tangu uanze kusoma hadi leo hujawai kufeli somo hata moja? Na unadhani waliofeli wote walikua hawapendi shule? Pia unafikiri kama walifeli ndio wamekuwa masikini? Hapana!! kufeli kule ndiko kulikowakumbusha umuhimu wa kufaulu, wakabadilika na sasa wamefanikiwa. Alafu fikiria kidogo, kama kungekua hakuna hasara nani angekua maskini? hata hao matajiri wenyewe wanapata hasara ndio maana wanahangika kutafuta faida. Hivyo basi HAKUNA BIASHARA ISIYO NA HASARA ILA DHUMUNI KUU LA KUFANYA BIASHARA NI KUPATA FAIDA, CHA MSINGI NI KUCHEZA SALAMA.
Baada ya frank kumaliza kuongea, darasa kwa mara nyingine likalipuka kwa kelele na makofi, loveness mwenyewe akashangaa, akajiiuliza huyu frank wa namna gani. Issa alikasirika sana alijua mipango yake imeharibika…….
MWL: wanafunzi utulivu utulivu, (mwalimu alionyesha kufurahi sanaa).
MWL: sidhani kama kuna haja ya maswali tena, na kutokana na majibu Mazuri ya frank hata kipindi changu kitaishia hapa. Swali lilikua nje ya somo letu lakini nimeshangaa sana jinsi lilivyojibiwa, ebu tumpigie tena makofi… (makofi na kelele zikalipuka tenaa)., sasa frank na loveness mnaweza kurudi kwenye viti vyenu…… na tutaonana tena kipindi kijacho, (mwalimu aliondoka).
Wanafunzi wakaanza kutoka darasani, kuna waliopitia kwa frank na kumpa ongera, walionekana na furaha sana, lakini issa alikasirika na kurudi hosteli haraka bila kuongea na mtu. Loveness yeye japo alikua na chuki lakin aliyaelewa majibu ya frank, alikua akiyatafakari sanaa.
Loveness akawa anatoka nje, akaangalia mahali alipokaa happy akamuona bado yupo akiongea na frank, alijiuliza “sasa huyu happy ameanza lini mazoea na frank au nae ameanza kujishaua”
LOVENESS: we happy fanya haraka twende!!!! (aliongea loveness akiwa kachukia kwelikweli)
HAPPY:  nakuja love, nisubiri kidogo... (aliongea happy akiwa anasimama).
Happy kabla hajaondoka, kwa siri sana akaficha kikaratasi kwenye daftari la frank alafu akaaga na kuondoka. Frank pasipokujua akakusanya daftari zake na kuziweka kwenye bag, alafu akaanza kutoka kuelekea hosteli.
********************************
Issa akiwa hostel alionekana kukasirika sana, akachukua simu yake, kuna namba alionekana kuitafuta, badae akaipiga ile namba, ikaitaaa na kupokelewa, akaanza kuongea, “oyaa kumeharibika tena……. eeh jamaa sifa zile zile, sasa tunafanyaje au we unaona fresh tuu? …ndo hapo sasa mi mwenyewe ningekuwa na uwezo wa kumuondoa chuo mbona saiz tungekua tushamsahau, ………sasa sikiliza week ijayo si kuna pepa basi tufanye kitu. …….…. eeh yan tuhakikishe ye ndo anakuwa wa mwisho darasa zima. Alafu unajua mchongo tuanze vip? .... tuanze na kile ki bag chake cha daftari maana jamaa uwa anapenda kuandika notice na anategemea sana zile daftar zake, ………eeh kaka huu mchezo tufanye mapema, ……… poa kaka” (alimaliza kuongea issa huku akionekana kujisifu mule ndani)
********************************
Frank Alipofika hostel akafikia kwenye godoro. Aliataka alale kidogo lakin ghafla akawa kama ameshtuka hivi “ooh week ijayo nina pepa la uchumi alafu nataka kulala, kwa raha zipi” alijisemea frank huku akiamka na kutoa daftar zake ili asome. Akatoa daftar moja na kuanza kulipitia, alionekana kama kuna kitu anatafuta… akajisemea “mbona zile notice sizioni, au sio daftari hili” akavuta bag na kutoa daftari lingine nalo akaanza kupekua, katika kupekua pekua akakuta kikaratasi kimekujwa, akakichukua na kukifungua akakuta kimeandikwa hivi…” nimependa sana jinsi ulivolijibu lile swali, nilishindwa kusema lolote mule ndani, ongera sana, nakuomba nitafute kupitia namba hii 0********* ni muhimu sana by happy”. (frank alimaliza kusoma ule ujumbe, lakini hakujua uyo happy ni yupi, hakujua kama ni yule aliekaa nae siti moja ila alijua tu atakuwa anasoma nae darasa moja, aliamua kuichukua ile namba akasave kwenye simu yake na kujiambia mwenyewe “badae nitamtafuta kwa sasa wacha nisome”).
********************************
ILIKUA NI MIDA YA JIONI, Happy alikua yupo kitandani akijigeuza geuza, mara ajiongeleshe mwenyewe “mh mbona hanipigii au bado hajaipata ile karatasi, au kaamua kuipotezea tu, ningejua ningemuomba namba yake maana natamani kama nipae hivi jamani” akiwa anaendelea kujigeuza pale kwenye godoro mara simu yake ikaita, akatoa tabasam na kuinuka ghafla kwenda kuichukua huku moyoni akijua lazma atakua ni frank, alinyong’onyea sana na kukasirika baada ya kukuta anayempigia ni loveness, akaitupa simu kwenye godoro, akajisemea “ huyu nae sijui anataka nini, sasa sipokei”
Simu iliita weee hadi ikakata, ikapigwa tena, happy akaona bora apokee
LOVENESS: we happy mbn hupokei simu?
HAPPY: nilitoka na simu niliacha room! (alidanganya happy)
LOVENESS: vp hatuendi kusoma venue?
HAPPY: tangulia tu mi nitakuja, saiz sina mood
LOVENESS: huna mood? Tangu lini? Twende bwanaa!
HAPPY: Kweli tenaa yan nimechoka sanaa.
LOVENESS: mh sawa utanikuta. (aliongea loveness na kukata simu).
Happy alifurahi, akaona kama loveness anamsumbua tu. Ye mawazo yake yote yalikua kwa frank, kuna mda aliamua kupiga magoti na kusali ili tu apigiwe simu na frank, akashuka kitandani huku akijisemea “maombi nayo yanalipa” akapiga magoti chini alafu akaanza kujisemea” eeh mungu hata sijielewi, ni ghafla tu nimejikuta napenda, nakuomba mungu wangu fanya hata miujiza ilimradi anipigie hata simu, pia………” kabla hajamaliza kusali akasikia simu yake inaita, akaacha na kusali kwenyewe akaifuata simu kuchek moyo wake ukapiga paa, ilikua ni namba ngeni moyoni akajisemea “eeh mungu na iwe kama nilivokuomba” alafu Akapokea simu,
“Hallow” (upande wa pili uliongea)
HAPPY: eeh hallo, sorry naongea na nani? (alijibu happy huku akiomba awe frank).
“Unaongea na frank” (ulijibu upande wa pili)
Moyo wa happy haukuamini, ulikua ni kama umeshtuliwa vile., happy nusura ajirushe pale kitandani, akainuka na kuiset sauti yake maana alichokitaka kilimjia….
HAPPY: ooh frank, nambie mzima lkn? (alikua ashalegeza sauti)
FRANK: yah mi niko poa tu sijui ww, ila sijakufaham bado.
HAPPY: mi ni happy, niliehamishwa siti nikakaa na wewe kwenye kipindi cha uchumi.
FRANK: AAH nishakukumbuka, vp kwema?
HAPPY: ndio kwema, lakinii, yah kwemaa! (aliongea happy kwa kubabaika)
FRANK: vp mbona hivo, kama kuna shida nambie tu!!! (happy baada ya kusikia hivo angalau akapata nguvu)
HAPPY: ni kweli nina shida. Naomba uje unielekeze uchumi kuna vitu sivielewi kabisa.
FRANK: sawa haina tatizo, upo wap?
HAPPY: niko hostel, room namba 43. (aliongea happy kimitego akiwa anajaribu bahati yake).
FRANK: mh sitoweza kuja hostel kwenu, labda twende venue!
HAPPY: hata mimi nilitamani tungeenda venue, ila najisikia homa kwa mbali ndio maana nimeona bora nisome room! (aliongea happy kwa kudeka).
FRANK: duh kwahyo tunafanyaje maana huko Siwez kuja. Nisamehe tu.
HAPPY: mmh kwan ww upo wap
FRANK: nipo room nasoma
HAPPY: upo na nani?
FRANK: nipo mwenyewe.
HAPPY: (akiwa anatabasam baada ya kusikia frank yupo pekeake hostel). Basi mimi nije huko kwako?
FRANK: (akafikiria kwamba amkubalie au?). poa kama unaweza njoo tu room 108!
Lakini frank akawa anajiuliza “si amesema anaumwa, amekataa kwenda venue kisa anaumwa, mbona huku anaweza kuja. Mambo ya wadada bhana, alafu usikute anatania tuu, hawez kuja itakua ananitania) …. wakati frank akiendelea kuwaza mara akasikia mlango unagongwa, akasikilizia kidogo akaona bado unagongwa….
Akasimama na kwenda kufungua , ile anafungua tu, macho kwa macho na binti mrembo ambaye alipendezwa aswaa!!!!!!!

Episode 05.

Chini alivaa sketi nyekundu alafu juu akapiga kigauni kifupi cheupe, ukizingatia na mguu wa bia pale chini weeh ama kweli alijipanga.
FRANK: ooh happy karibu sanaa (huku akimtatazama vizuri kabisa kwa uzuri wa happy, lakin akajiambia moyoni kuwa ameshazoea hali ile kwa wanachuo wa kike wengi tu, akajidai kupotozea)
HAPPY: asante nishakaribia. (akaingia na kwenda kukaa kwenye godoro wakati Kulikua na viti viwili mule ndani).
Baada ya happy kuingia, frank akavuta vile viti akaviweka sawa mbele ya meza ya kusomea. Alafu akamkaribisha happy
FRANK: happy?
HAPPY: abee!
FRANK: karibu ukae kwenye kiti ili tuanze kusoma, au vp
HAPPY: ok sawa hakuna tatizo… (huku akiinuka kichovu alionekana kama hapendi kutolewa kwenye lile godoro, alilaani sana uwepo wa vile viti).
Basi alikaa, frank nae akakaa teyari kwa kusoma.
FRANK: ni sehemu ipi unataka nikulekeze?
HAPPY: (alifikiria akijua kuwa hajafuata kusoma ila basi tu, akafikiria topic ngumu ambayo hakuwai kuisoma) naomba unielekeze kuhusu tabia za wateja katika biashara
FRANK: ooh sawa haina shida, vp umekuja na daftari lolote?
HAPPY: aah hapana, sorry nilisahau.
FRANK: (akawaza “sasa atakujaje kuelekezwa bila daftari, huyu happy vp) ok usijal, nitatumia langu alafu utaenda ku coppy.
HAPPY: sawa asante sana
Frank akavuta bag lake na kutoa daftar flan ambalo halikuandikwa kitu zaid ya jina, akaweka mezani na kuanza ualimu, akamkumbusha happy kusikiliza na kuwa makini….
FRANK: “wateja ndio kitu cha kwanza na chamsingi katika biashara ukiondoa bidhaa. Hapa namaanisha ili uwe mfanyabiashara lazima ujue utafanya biashara gani Mfano kama kuuza utauza bidhaa gani, ukishafahamu bidhaa yako ni ipi kinachofuata hapo ni kutafuta wateja.  Waenga zamani walisema “kizuri chajiuza kibaya chajitembeza” hapa walimaanisha ukiuza bidhaa nzuri wateja watakufuata wenyewe. Na msemo huu uwa unatumika sana pale ambapo watu wengi wanauza biashara ya namna moja (inayofanana). Ikitokea bidhaa zikiwa zinafanana hata kama zote ziwe bora, mteja atachagua kule kwenye kizuri kunakomvutia. lakini msemo huu katika ulimwengu wa sasa hautumiki sana kwa sababu wateja wengi hawamfwati muuzaji ila muuzaji anatafuta wateja kupitia matangazo, punguzo, nyongeza ya bidhaa, maneno mazuri na ushirikiano na wateja wako pamoja na bei ya kawaida. Mtu unaweza kuwa na bidhaa nzuri lkn usipozipa matangazo, punguzo n.k hutoweza kupata wateja. wao wanafuata kule kutakowapa motisha, kule ambako kile wanachokilipa kitafanana na kile wanachokipata. (fedha yao wanayolipa ifanane na thamani ya bidhaa wanazonunua). Mteja lazma aridhike, wateja wanapenda sana kuchagua, hivyo basi ni muhimu mfanya biashara awe na bidhaa mchanganyiko ili mteja achague anachokitaka. Lakini wateja hawa wapo tofauti, kuna wale waongeaji na wengine hawajui kuongea, kuna wengine ni ngumu kuwaridhisha hivyo basi inabidi utambue tabia za wateja wako.” Vipi unanielewa happy?
HAPPY: (kiukweli happy hakuja kusoma lakini kutokana na maelezo ya frank alijikuta anasikiliza kwa makini na alionekana kunogewa sana, ushawishi wa frank katika kusoma ulimfanya happy atulie na asahau kwa muda mambo ya mapenzi, happy alijiona yupo katika mikono salama, hakika alimpenda frank kwa kila kitu.)” Yaah nimekuelewa tena sana frank, naamin pepa haitotoka nje ya hapa?
FRANK: ni kwel ila Usisahau kusoma na topic zingine
HAPPY: sawa! Nimechoka nataman kama nilale kidogo, alaf tuendelee au
FRANK: (akacheki saa yake ilikua ni saa 2 usiku). Mi naona tuishie hapa kwa leo, Kwakuwa pepa ni wiki ijayo, basi kesho tutaendelea.
HAPPY: sawa frank asante sana. Mi nikuache bas
FRANK: sawa usijar tutawasiliana. (happy Aliaga na kutoka, moyoni alijikuta amependa ghafla ila kusema ndo ilikua tatizo, alijiapiza tu lazma ampate frank).
Happy alivyokua anatoka mlango wa nje wa hostel alipishana na issa, Kwakuwa hawakuzoeana walipishana tu, lakin issa alikua anamjua happy kama ni Rafiki wa loveness, akajiiuliza “huyu si rafiki wa love huyu, humu ndani anatokea room gan au kuna jamaa anabeba mzigo nini” hakupata majibu…
********************************
issa alivoingia hostel hakwenda room kwake, aliingia room flani hivi akakutana na Rafiki ake
“kaka vip” aliongea issa
“Fresh inakuaje” alijibu yule Rafiki ake ambaye alifahamika kwa jina la Meshack
ISSA:  nimekuja tukamilishe mchongo tujue tunafanyaje
MESHACK: aah si mchongo kuhusu yule mpenda sifa au?
ISSA: huyo huyooo, silipendi lijamaa lile!
MESHACK: sasa rahisi tu, inabid tuwe washkaji kama wanne hivi, tunatengeneza swali la uongo, alafu tunamtumia tukimsisitiza hilo ndo swali litakalotoka kwenye test, we mwenyewe unajua hakuna asiyependa possible (nondo), akitumiwa na watu wanne ataamini tu.
ISSA: (akiwa na wasiwasi). Mh mbona naona kama ngumu, sasa si atauliza watu wengine kama nao wamelipata?
MESHACK: hawez, kwenye hiyo meseji tunamsisitiza akishaipata akae kimya kwasababu kila mtu ametumiwa. Alafu si unajua yule jamaa hayupo hata kwenye group la WhatsApp?
ISSA: eeh hayupo, hapendag mambo ya kuchat yule
MESHACK: sasa hapo ndo penyewe, hana wa kumuuliza. Akishapewa swali ataangaika nalo kulisoma alafu kwenye pepa anakutana na mziki mwingine….
ISSA: nimekupata, kwahyo si tunaanza na lile bag lake au vp?
MESHACK: lile bag si fasta tu, tunamvizia mda akienda kuoga, alafu na akishaibiwa bag si atachanganyikiwa, atakuwa hana notice za kusoma, hapo sasa lazima atalisoma tu lile swali tutakalomtumia, huyu dawa yake ni kumpumbaza akili, asiwaze vitu vingine zaid ya hilo swali tu.
ISSA: mwanangu ebu nipe tano (wakagongesheana mikono kwamba dili limekubali).
********************************
Basi siku ikapita, na ikawa ni jumamosi ya wiki mida ya asubuhi. Wanafunzi wengi walionekana wako busy na kusoma, wanafunzi wa biashara nao walishaanza kujiandaa na pepa ya uchumi ambayo itafanyika jumatatu ya wiki inayokuja. Inamaana zilikua zimebaki siku mbili, hiyo jumamosi na jumapili.
Loveness alikua room pamoja na happy wakijisomea. Kila mmoja alikua busy na daftari lake, happy alikua akisoma huku akimuwaza frank, kuna muda alitabasam, na kuna muda alicheka kabisa pekeake
LOVENESS: we unacheka cheka nini?
HAPPY: hakuna, basi tu
LOVENESS: mmh, alafu mwenzangu siku mbili hizi hata sikuelew, umepata bwana nini? (aliuliza love akiwa anatabasam)
HAPPY: mbona ningempata ningefurah
LOVENESS: ungempata nan?
HAPPY: si huyo bwana
LOVENESS: ni nan huyo nisiemjua?
HAPPY: nakutania mwaya!!!!
LOVENESS: mmh sawa. Sasa kuna hichi kiswali naomba unielekeze kama unakijua
Happy alilicheck lile swali akalisoma lilikua hivi “elezea tabia za wateja katika biashara”. Alitabasam baada ya kukumbuka ni jana yake tu alielekezwa na frank. Akaona huo ndo mda wa kumuonyesha happy kama anajua kwelikweli….
Basi wakaweka daftari kwenye meza, loveness alipewa somo, nae happy alipita mule mule kama alivyoelekezwa na frank mpaka happy akaanza kushangaa…….
LOVENESS: we happy, haya mambo yote umeyajulia wap?
HAPPY: si kujisomea jaman (huku akitabasam)
LOVENESS: wee kwenda zako muda wote tunakuaga wote, sasa uko kujisomea vepe?
HAPPY: ndo hivyo, au hujaelewa nirudie?
LOVENESS: sijawai kukuelewa kama leo. Yaan ujue bado sikupatii picha….
HAPPY: (akajichekesha tuuuuu, ukweli aliujua mwenyewe ila aliogopa kusema amefundishwa na frank)
********************************
Jumamosi ile Frank alichelewa kuamka, akajikuta ameamka saa 3, akatazama godoro la juu yake hakuona mtu, (yeye anakaa room na mtu ambaye anasoma kozi tofauti na yeye) “aah alisema leo jumamosi ana kipindi saa 2 mwalimu kawaomba”.  Alijisemea frank…
Basi Akakaa kitandani na kumshukuru mungu kwa kumpa afya na uzima wa kuiona siku mpya, baada ya hapo akachukua mswaki wake na kutoka nao nje kwenye kalo la kunawia maji, akapiga mswaki na kurudi ndani, akachukua taulo lake na ndoo akaelekea bafuni ili akaoge.
Ile anatoka tu, issa na Meshack wakazama room kwake haraka, baada ya dakika 2 wakatoka.
Frank akamaliza kuoga, akarudi room kwake bila wasiwasi wowote. Akajifuta maji vizuri na kupaka mafuta. Akapiga pamba zake na kujiona yuko teyari kwenda kujisomea., lakini kabla hajaondoka akatandika vizuri godoro lake na kuweka nguo vizuri kwenye kabati. “hapo sasa ruksa niondoke” akajisemea uku akitazama bag lake anapoliwekaga…
Ile kucheck ukutani begi halionekaniiii…….

Inaendelea..

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01

TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01