TAMTHILIA: MOON OF MY LIFE (MML) sehemu ya kwanza

TAMTHILIA: MOON OF MY LIFE (MML)
Mtunzi/mwandishi: manshye
***************************************
Episode 01

Ni baada ya kumaliza chuo, kijana aliekuwa mtu pendwa chuoni kutokana na utanashati wake, akili yake ya darasani na kujitambua kimaisha, upendo na ushirikiano wake kwa vijana wenzie wa jinsia zote, upole, ukarimu na uchangamfu wake kutokana na mazingira zilikuwa sababu tosha za mtu huyo kupendwa. Licha ya sababu nyingi, walizoea kumuita handsome boy kutokana na sura yake na staili ya nywele zake kufanana na mcheza mpira wa miguu maarufu kwa jina la neymar jr pamoja na muigizaji maarufu wa bongo movie aitwaye rammy galis, hata yeye mwenyewe aliwapenda sana hao watu. Lakini pia alishawai kuitwa fonsi, hii ni kutokana pia na stahili na mbwembwe zake kufanana na muimba muziki wa nchini pueto rico, luis fonsi, aliyetamba na wimbo wa despacito, Kijana huyo sio mwingine bali ni kaxoghur santos jr.
Sifa zake hazikuishia chuoni, hata mara baada ya kurudi kwao dar es salaam, vijana wengi hasa warembo walitokea kumpenda sana, alipendwa kweli kweli. Wapo waliompenda kwa upendo wa kawaida, wapo waliompenda kirafiki lakini pia kuna waliompenda kimapenzi, wadada wengi waliangaika kwaajili yake wakitaka kuwa nae kimahusiano ya kimapenzi lakini kaxoghur wala hakuwa na mpango nao, tena hakuonyesha dalili zozote kwao.
Lakini pia licha ya kuhitimu shahada ya utawala wa biashara (business administration) na kufahulu vizuri hakutaka kuangaika sana na ajira, yeye kila akiamka asubuhi kazi yake ilikuwa ni kuchukua daftari na kuandika mipango yake ya kimaisha hasa kuhusu biashara, anataka kuwa nani, ataanzaje anzaje, namna ya kupata mtaji na namna ya kuimiliki biashara. Kauli yake kubwa ilikuwa ni “ mjasiriamali bora ni yule anaekuja kuwa mfanyabiashara, kwasababu biashara ni hatua ya kijasiriamali”
Licha ya yeye kuwasumbua baadhi ya mabinti kimapenzi, lakini yeye pia moyo wake ulianza kupenda na kusumbuka kutokana na binti mmoja wa hadhi ya juu ambae alikuwa akikaa nae mtaa mmoja. Binti huyo mrembo, ambae aliwatesa vijana wengi sana mtaani kwake kutokana na umaarufu wake, urembo wake ambao ulishawafanya baadhi ya wasanii kuvutika nae, alishausishwa kutoka kimapenzi na wasanii wakubwa kama diamond platnumz, harmonize n.k, japo haikuwa kweli. maringo yake yaliyofanya vijana mtaani wamuogope ni kutokana na huo umaarufu, vijana wakidai sio levo yao, hakupenda sana kujihusisha na mitaa, maisha yake yalikuwa ya juu, ni binti mdogo mdogo tu wa miaka 18 ambae kwa muda huo alikuwa akisoma kidato cha nne, lakini maisha aliyokuwa akiishi ni Zaidi ya chuo kikuu , yeye ni mtoto pekee na pendwa wa mwigizaji wa bongo kajala masanja na mtengenezaji wa muziki nchini Tanzania, paul matthysse almaarufu kama p. funk majani, binti huyo sio mwingine bali ni “paula”, paula kajala.
******************************************************
Siku moja kaxoghur akiwa kijiweni na marafiki zake mara wakamuona paula akiwa na mama wakiingia kwenye gari, mazungumzo yakaanza…
“dem namchukia yule”…aliongea mpita
KAXOUGHUR: kwanini unamchukia?
MPITA: aah mtu anaringaaa utadhani kitaa mzuri ni yeye tu…
“ila kweli asee, yani mi sikuhiyo kumuita tu hata kugeuka hakugeuka” aliongea jamaa mwingine  mandingo
“mimi jana tu, nilijaribu kumsalimia akanifyonya, nikaona ushenzi nikaachana nae ” huyo sasa ni kitalo
“madem wengine hadi wabakwe ndo watakuelewa” aliongea ade
MANDINGO: lakini tuseme na ukweli, yule demu ni mzuri jamani, kama malaika…!!!
MPITA: kwa uzuri sawa ni mzuri, lakini ndo aachage maringo yakiwaki…sisi ndo wahuni wa kitaa chake, lazma agawe
KITALO: ona kwanza lile paja, mguu mweupeee, dah wakubwa wanafaidi asee…
ADE: sio wakubwa, yule manzi hata mi nikiamua napiga, sema tu bado mtoto, tusubiri akue…
MPITA: mtoto kwakuwa anasoma sekondari? unazingua, yule anapigwa, angalia tu ule mbinuko kule nyuma… sema tu yule manzi ndo hivo hatumuwezi, life yake ya juu na mtu mwenyewe kumuona kwa nadra, mtoto geti kali…….
KAXOGHUR: sasa sikilizeni, yule manzi mi lazma akae na atakuwa shemeji yenu,……
“Ah ah ah dadeq” walimcheka kwa kumdharau.
**********************************************************
Paula nae siku flani akiwa na marafiki zake, nje tu ya nyumba yao kulikuwa na mti mkubwa wenye kivuli kizuri, basi siku akijiskia au akitembelewa na marafiki uwa wanapenda kukaa mahali hapo kwaajili ya stori, siku hiyo wakiwa nje kwenye huo mti mara akapita kaxoghur ambae alivaa nadhifu kama kijana anaejitambua na kujijali, maneno ya upembuzi yakaanza…
“ila yule kaka mi nampenda jamani” aliongea binti mrembo “Tabitha”
“yani yule anaringa kama nini, tangia kamaliza chuo anajiskia balaa, nishawai kumjaribu lakini hata hasomeki” huyo sasa alikuwa Sandra
“ mi mwenyewe namchukia, japo anawasaidia watu wengi kupitia biashara lakini amezidisha kujiona” aliongea Josephine
PAULA: nani alimsaidia?
JOSEPHINE: wengi tu, wengine ni watu wa makampuni, bodaboda, wauza vyakula, kila ukipita mtaani wafanyabiashara wanamsifia…
SANDRA: na anaonekana ana mawazo ya mbele sana, we muone tu hata mwendo wake…
JOSEPHINE: sema ndo hivyo tu kujisikia kumezidi looh
TABITHA: hata kama lakini mimi nampenda tu..
SANDRA: lakini pia japo tunamsema vibaya, ila ni handsome jamani mmh!!!
JOSEPHINE: mi napendaga nywele zake, anavotembea kwa kujiamini na mapozi, pia jinsi alivo mwanaharakati..
PAULA: mnamsifia tu, hana lolote, siwezi kuwa na mwanaume wa hivyo…
“Ah ah ah makubwa” walicheka wenzake
*************************************************************
Siku zikapita kaxoghur akiendelea kujiweka vizuri kwenye suala zima la mipango ya kimaisha yake hasa kupitia biashara, alijikubali sana kwamba akiamua kufanya kitu anaweza, alishatumiwa sana na biashara za watu kiushauri na mawazo mbalimbali ya biashara.
Ilkuwa ni siku ya jumamosi baada ya kutoka nyumbani kwao akaona azunguke kidogo mtaani kwa ajili ya kufanya uchunguzi wake wa kibiashara kwa kuangalia huduma muhimu zinazokosekana mtaani kwao hili ajue nini cha kufanya. Sasa katika pita pita, mara akakutana na paula akiwa pekeake, akaona muda ndo huo, akamuita….
KAXOGHUR: hello paula……
Lakini paula kama kawaida yake licha ya kumtambua vizuri kaxoghur kutokana na rafiki zake kumsifia sana siku za nyuma lakini hakusimama wala kujibu wala kumtizama kaxoghur usoni, alimpita na kusonga mbele…kaxoghur akageuka nyuma kumtizama..
KAXOGHUR: lakini sio lazima sana kwa mfanyabiashara aangaike kumvuta mteja, mteja pia anapaswa kutambua, bidhaa bora aliyoiona anaihitaji na hasiiache……
Paula baada ya kusikia hivo akashtuka, hakujua maana yake lakini alihisi lazma anaambiwa yeye, akajikuta anageuka na macho yake kukutana na yale ya kaxoghur yakimtazama, kaxoghur akamsogelea hadi pale alipo…
KAXOGHUR: vipi?
PAULA: kauli yako ina maana gani?
KAXOGHUR: wewe sio mfanyabiashara, sidhani kama maneno haya yanakuhusu…
PAULA: kwahiyo ulikuwa ukimwambia nani?
KAXOGHUR: mjasiriamali, nilikuwa namkumbusha tu, hili awe na muhusiano mazuri kwa mteja wake, mawasiliano ni muhimu….
PAULA: huyo mfanyabiashara ni nani? na huyo mteja ni nani? Eleweka basi…..
KAXOGHUR: je wataka kuwajua? Nipe mawasiliano yako…
PAULA: (akafyonya), eti mawasiliano, uwasiliane na nani? Ebu jitathmini sio kila ukionacho unaweza kukipata, huna hadhi ya kuwa na namba yangu….
Paula akaondoka kwa nyodo akimuacha kaxoghur akimtafakari, kaxoghur akamtazama sana paula akajiliwaza kwamba sio mbaya, inawezekana kama akijaribu tena, kama walisema huwa hasimami nay eye amemsimamisha , ipo siku anachokitaka kwa mrembo huyo atakipata.
lakini vile anakuja kugeuka akashangaa kukutana macho kwa macho na marafiki zake wakiwa wanamcheka…
MPITA: hivi wewe kwa akili zako finyu unazani unaweza ukampata yule?
MANDINGO: au anadhani yule ni sawa na videm vyake vya uswazi, ah ah ah
KITALO: na bora tumemuona akisutwa maana tusingemuona angekuja kutudanganya, mara hivi, mara vile ah ah ah
ADE: lakini muacheni labda anaweza kubahatisha, maana madem wengine bila bahati huwapati, au sio mwanangu fonsi? (akiwa anacheka kwa masihara)…..
KAXOGHUR: sawa nyie nichekeni lakini ipo siku…
MANDINGO: siku ya kutukanwa au sio?
KITALO: au siku ya kuaibishwa mbele za watu, maana watoto wakishua wale popote wanakuumbua…
KAXOGHUR: tuache habari hizo, twenzao kijiwe nikawapige draft?
MPITA: ah ah ah leo utatamani hata kucheza mpira wa kikapu.
***********************************************************
Bado hakuridhika na majibu ya mwanzo, siku nyingine tena kaxoghur akiwa anaangalia mpira na ndugu zake kwenye kibanda umiza, mara baada ya kuangalia nje akamuona paula akishuka kwenye gari na ile gari ikaondoka, anaifaham vizuri nigari ya mama yake paula, hakujua paula yupo maeneo hayo kwa ajili gani, akaona bora aachane na mpira, akatoka akiwaacha wenzie wakimtazama kwa unafki…akasogea hadi pale alipo paula alafu akaita..
KAXOGHUR: mfanyabiashara….
Paula akashtuka, alishahisi ni mtu gani, akageuka
KAXOGHUR: mambo…
PAULA: mabaya, alafu acha kunifuatilia….
akataka kuondoka, lakini kaxoghur akamshika mkono, paula alichukia na ukizingatia yeye ana heshima zake kutokana na mama msanii, pia anajulikana sana, hawezi kushikwa kirahisi na mtu ambae sio wa hadhi yake, mtu ambae hajulikani hata chanzo chake, kwa jicho kali la dharau akamtazama kaxoghur ambae wala hakuonyesha kuogopa, paula kwa nguvu akauvuta mkono wake kutoka kwa kaxoghur, alafu akarudi nyuma kidogo…
PAULA: wewe kimtu jiangalie, tena jitazame kuanzia juu, katikati hadi chini, nyie vibaka sijui mkoje, ndo stahili yenu hii ya kuwaibia watu sio? Mtu humjui, umemuona tu unaanza kumfuatafuata utadhani alikuzaa, mbona nyie wabongo mna mambo ya kuja sana? Hivi unadhani kila mtu anazoeleka? Au kukaa mtaa mmoja na wewe ndo kwamba tunaweza kufahamiana? Thubutu, kwanza hizo ndoto futa, muone midevu yake ilokosa matunzo, sasa endelea kunisumbua ndo utanitambua…..
Alifunguka kwa hasira binti paula, toto wa kidato cha nne ambae alisumbua wababa wa maofisi ya umma,binafsi, wafanyabiashara, wanachuo na hata wale wa mitaani. Alijiamini sana kutokana na maisha yake ambayo yalikuwa hayana hata chembechembe za shida. Kuna baadhi ya watu walikuwa wakishuhudia tukio lile ambalo licha ya kaxoghur kupewa makavu lakini bado alitabasam na kumtazama paula usoni, kisha akamwambia..
KAXOUGHUR: ni ngumu sana kwa mteja kuitambua bidhaa bora, hii ni kutokana na sababu tofauti tofauti ikiwemo ujinga wa kuto kujitambua…….
PAULA: nini?

USIKOSE SEHEM YA PILI......

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01

TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01