SIRI YA MAFANIKIO

JIAMINI, WEWE NI SABABU.

Ukiusikiliza wimbo wa HARMONIZE -NEVER GIVE UP kuna sehemu utasikia akisimulia namna alivyoenda kushindana katika mashindano ya kuimba ya BONGO STAR SEARCH (BSS)  na akaambiwa hajui kuimba.

inaonekana harmonize mwenyewe alijiamini kwamba anajua Sana kuimba,  lakini waliomsikiliza walaikataa wakidai hajui.

LAKINI,  Leo hii HARMONIZE akitoa nyimbo hata wale waliokuwa wakimdharau kuwa hajui,  wanacheza nyimbo zake na wanatamani kuwa Kama harmonize .

NDIVYO ILIVYO;  katika haya maisha ni ngumu Sana mtu kuamini kipaji au uwezo wako. Hata Kama wewe mwenyewe unajiamini na unajikubali lakini ukiwaonyesha watu kwamba unauwezo flani, hawatokuamini, watakuambia unapoteza mda,  hufai.

HATA kwa wajasiriamali,  mwanzo uwa mgumu Sana,  utakuta kuanzia wajasiriamali wenzio, wateja hata wapita njia WOTE HAWAKUAMINI,  tena wengine wataona hufai kuwa mjasiriamali.

KUMBUKA;  ukiruhusu tu kuwapa nafasi katika akili yako UMEKWISHA,  UMEPOTEA,  HUO NDIO UTAKUWA MWISHO WAKO.

MARA NYINGI,  mtu uonekana wa maana pale akishaanza kufanya mambo makubwa, na siku zote hata ukiwa na makosa lakini ukiwa mkubwa KOSA HALITOONEKANA.

sio kwamba harmonize wa SASA ana utofauti na yule BSS,  hapana, harmonize ni Yule Yule,   ila kwasababu harmonize wa Leo ni maarufu,  Ana pesa kuzidi zamani hivyo basi LOLOTE ATAKALO FANYA NI ZURI,  HALIKOSOLEWI.

KUMBE kukosolewa inategemea upo katika NAFASI GANI.

Alichokifanya harmonize ni kujitengeneza kuwa mkubwa.

TUAMBIZANE KITU:
kumdharau mtu aliyeumbwa kwa kusudi la mwenyezi mungu ni KOSA KUBWA.  kumdharau mtu husiejua kesho atakuwa Nani,  ni KOSA.

UJUMBE: tujitengenezee mazingira mazuri,  mazingira ambayo wale wanaotuchukia Leo wataumbuka kesho.

By manshine
INSTAGRAM: manshynee

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01

TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01