TAMTHILIA: CPL (CERTIFIED PERSON OF MY LIFE) sehemu ya 01


TAMTHILIA: CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (CPL)
(MTU ALIETHIBITISHWA KWA MAISHA YANGU)
MWANDISHI: MANSHINE
Email address: manshinef@gmail.com
instagram: @manshynee          facebook @let us shine

Episode 01.
VENUE:
Ilikua ni muda wa kipindi cha ujasiriamali kwa wanafunzi wanaosomea biashara., lecturer (mwalimu wa chuo) akiwa mbele ya venue akifundisha. Kutokana na ukali wa lecturer yule darasa lilikua kimya sana hali iliyopelekea wanachuo kuwa waoga kwasababu walishaambiwa katika kipindi chake kuleta fujo au kelele ni sawa na kujiondoa chuoni hapo.
Frank akiwa ni mmoja wa wanachuo alikua makini sana kusikiliza. Ilifikia hatua akawa anatikisa kichwa kuonyesha jinsi gani alikua akielewa katika kipindi hicho. Wakati kipindi kikikaribia kuisha, mkufunzi (lecturer) aliuliza swali…
“wanafunzi Nani anapenda kuwa mfanyabiashara., na kwanini? Na mtaji utaupata wapi?
loveness akanyosha mkono, akaambiwa ajibu swali…
LOVENESS: mimi sipendi kuwa mfanyabiashara kwasababu biashara zina hasara nyingi, ni ngumu kupata mtaji kwa sababu watu wengi wanaitaji fedha na fedha ni ngumu kupatikana. Kabla mwalimu hajaongea chochote akaona mkono wa frank….
MWALIMU: eeh frank nawe una jibu jipya? Ebu tupe jibu lako
FRANK: mwalimu nataka nimjibu loveness, loveness unaposema hupendi kuwa mfanyabiashara una maana gani? Na kama hupendi tuambie kwanini unasomea biashara?
LOVENESS: mfanyabiashara ni sawa na mtu aliejiajili, sasa mimi nikijiajiri kuna faida gani za kusoma sasa? Si nitakua tu nimepoteza fedha zangu. Sasa si bora ningekaa nyumbani na hizo fedha za ada ningezitumia kama mtaji. Nasomea biashara kwa sababu serikali itanipa ajira zinazohusu usimamizi wa biashara za wananchi.
FRANK: HAPANA, kumbe una mawazo finyu hivo. Tena wewe mwanachuo wa elimu ya juu unaweza ukatupatia majibu kama hayo? Hata hiyo serikali haiwezi ikakuamini kwasababu huwez ukaongoza wafanyabiashara wakati hupendi biashara.
LOVENESS: kwani tatizo lipo wap? Jaman kila mtu ana ndoto zake. Humu ndani kuna watu wanawaza kujiajiri na kuna wengine akina sisi hatuna mpango huo. Mimi nachoamin baada ya ku graduate ni kusubili ajira tu. Na naamini nitaajiliwa. Siwez kupoteza muda wangu na fedha zangu bure hata wale wenzangu walioko uko mtaani si watanicheka?
FRANK: loveness kwanza serikali ni nini? Unataka kusema serikali haifanyi biashara? Hivi hujawai kusikia serikali inanunua au kuuza vitu kutoka nje? Tena ni juzi tu tumemaliza topic ya international trade, unataka kusema ile topic hukuilewa au?
LOVENESS: kwan wewe unataka nini? Kama unaona jibu langu sio sahihi basi tupe lako kwa sababu naona unapinga mawazo yangu. (aliongea loveness akiwa na uso wa hasira na akaamua kukaa chini)
FRANK: haina haja ya kupanic kwa sababu swali liko wazi kwa sisi wote ambao tunachukua biashara. Mimi sijamaanisha kwamba sitaki kuajiriwa au sijamkataza mtu kuajiriwa ila Kutokana na swali majibu ya dada etu love sidhani kama ni sahihi. Mwanachuo alie kamili kifikra hawez kutujibu vile…... (kabla frank hajamaliza kuongea loveness akasimama kwa hasira na kuongea)
LOVENESS: kwahyo mimi sina fikra, sifai kuwa mwanachuo, unaamua kuni…. (kabla hajamaliza kuongea akaanza kulia kwa kwikwi na akatoka nje kwa hasira bila hata kuangalia nyuma).
Kulikua na ukimya wa muda, kipindi hayo yote yanaendelea darasa lilikua kumya kusikiliza, kuna nyuso zilionyesha huruma kwa loveness na kuna nyuso ziliona ni kitu cha kawaida kimetokea…kwa upande wa frank alikua bado amesimama, alipotaka kukaa mwalimu akamwambia inabid alijibu swali kwa faida ya waliobaki…...
FRANK: Mimi napenda kuwa mfanyabiashara, hata kama ikitokea nikapata ajira selikalini lakin sitoacha kufanikisha ndoto zangu za kuwa mfanyabiashara na ndio maana niliamua kusomea kozi hii. Napenda biashara kwa sababu biashara iko popote iwe ni sekta za umma hata zile binafsi, ailimia 99% za vipato vya watu ni biashara. Kwa upande wangu biashara inatengenezwa na bidhaa pamoja na huduma za kijamii. Hivo basi hata serikali inatengenezwa na biashara.  Na kuhusu mtaji ni rahisi tu, kuna mikopo kutoka bank na mshirika yatoayo mikopo, kuna akiba, kuna misaada kutoka kwa watu wa karibu n.k
MWALIMU: safi sana, nadhani hakuna asiyekuelewa. Na hii inaonyesha ni jinsi gani una upeo wa kielimu hasa katika kozi yako ya biashara. Class see you next lecture. Aliaga mwalimu na akaondoka darasani….
Baada ya mwalimu kuondoka, huku nyuma yalibaki majadiliano kuhusu yaliyotokea, kuna waliosema frank amekosea sana kwa kumdhalilisha loveness, kuna waliosema frank ameongea sahihi. Ilikua ni kelele tu Kila mtu akiongea lake.
Baada ya muda watu wakaanza kutawanyika hadi frank akajikuta yuko pekeake mule ndani. Kwakuwa ilikua ni saa 6 mchana frank akaona ni bora ajisomee tu mule darasani hadi mida ya saa saba ndo akale chakula. Akatoa ki note book chake akaanza kukipitia, hakuwaza sana kuhusu yaliyotokea kwasababu aliona ameongea vitu ambavyo mtu yeyote angeweza kuongea. Akiwa yupo busy na kusoma mara akaingia Maria ambaye ni groupmate mwenzie.
MARIA: frank vipi mbona pekeako humu class?
FRANK: hamna nimeamua tu, nimeona nikiwa nasubir mda wa msosi, niwe napitia pitia kidogo.
MARIA: hivi una taarifa mwenzio kapelekwa hospital ya chuo?
FRANK: mwenzangu gani?
MARIA: si loveness baada ya kutoka class unaambiwa kaenda hostel na kilio, sie tumetoka pindi tunafika hostel tunamkuta mtu kazidiwa ilibidi tumuwaishe hospitali.
FRANK: (KWA MSHANGAO) eeh lakin si alikua poa tu. Amezidiwa kivipi?
MARIA: hospiali wanasema ni maumivu ya kichwa yalimzidi. Na inasemekana chanzo ni wewe?



USIKOSE SEHEMU YA PILI....

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TARATIBU ZA UCHUMBA KABLA YA NDOA.

CHOMBEZO: HISIA MBAYA sehemu ya 01